
Matokeo yake ni muhimu kuyatambua na kubadili aina hii ya mawazo. Lazima mawazo chanya yawe mazoea endelevu ya kiutendaji wa kiakili. Yanapaswa kuhusisha kila kipengele cha maisha.
Haya ni matokeo yanatakiwa kuzingatiwa
Mawazo chanya juu ya mtu binafsi.
Usijenge mtazamo-binafsi kwa kujilinganisha na wahusika wa luninga au filamu au watu katika Maisha ya umma au katika mitandao ya kijamii. Hivi huwasilisha taswira isiyo halisi. Tambua mapungufu yako, kisha chukua hatua Fulani ili kufanya maboresho binafsi. Hasa, usisahau kusisitiza maadili na uwezo wako. Kata mawazo ya kujidhuru.
Mawazo chanya kuhusu wakati uliopita.
Wakati uliopita hauwezi kubadilishwa. Tunapaswa kukubali hata matukio mabaya yaliyotokea. Usilaumu wakati uliopita kwa ajili ya hali mbaya zinazotokea leo. Hili halina manufaa yoyote kabisa. Usihofu kuhusu mambo yasiyopendeza yaliyotokea zamani. Zingatia furaha na mafanikio mengi ya jana, kumbuka na kuyafurahia, hapo ndipo mtazamo wako utakuwa chanya zaidi.
Mawazo chanya kuhusu wakati ujao.
Wakati ujao unaweza kubadilishwa, kwa hiyo mwenendo wako leo huathiri mafanikio yako ya kesho. Kufikiri kijasiri na kuwa na tumaini kutaongeza uwezekano wa Maisha yako yajayo yenye furaha. Na kama kuna kitu fulani kibaya kinachoweza kutokea, panga mapema ili fadhaa isikushtukize endapo kikitokea.
Mawazo chanya kuhusiana na mazingira na watu.
Vaa “Miwani ya uvumilivu” kisha tazama mazingira yako. Ingawa si kila kitu ni kamilifu, utapata baadhi ya mambo mazuri na uzoefu wa matukio ya kuvutia. Usiwahukumu watu lakini badala yake waheshimu na kuthamini mambo mema watendayo. Tafuta kuelewa matatizo yao na kuwasaidia. Kwa namna hii mwenendo wako utakuletea ridhaa.
Soma nukuu hizi toka kitabu cha dini
Msitende neno lolote kwa kushindana wala kwa majivuno; bali kwa unyenyekevu, kila mtu amhesabu mwenziwe bora kuliko nafsi yake
Basi farijianeni na kujengana kila mtu na mwenzake
Wakati mwingine baadhi ya watu hujiruhusu kutawaliwa na mawazo yasiyokuwa na mantiki. Mawazo haya husababisha huzuni na vikwazo.
Hii hapa baadhi ya mifano:
“Tumezungukwa na matatizo na hatari daima, n ani jambo la kawaida kwetu kuhofu na kuogopa”
“Watu ambao ni wahitaji na wenye huzuni hawawezi kufanya lolote ili kuboresha hali zao”
“Ili kuwa na furaha na kuishi kwa amani na nafsi yangu, nahitaji kupata ukubali na upendo wa kila mmoja anijuaye”
“Wakati wote kuna ufumbuzi kamili wa kila tatizo, na endapo ufumbuzi huu usipofikiwa matokeo yatakuwa madhara makubwa”
Kauli hizo hapo juu ni udanganyifu. Kukubaliana nazo huweza kuleta maumivu ya kisaikolojia na huzuni. Unapaswa kufanya juhudi ya kutamua na kuchanganua mawazo yako yasiyo sahihi. Fikiria kwa makini ili uweze kuyakataa na kukubali zingine mbadala ambazo ni bora.
Wapo watu wanaoamini kwamba raha na furaha hutokea kwa nasibu, kwamba hii hauthiriwa na mazingira au ni masuala ya bahati. Hata hivyo, mara nyingi sana, raha na fuaraha huapatikana kwa chaguzi binafsi. Kuwa na fuaraha ni suala la uamuzi. Baadhi ya watu huchagua kuwa na mtazamo chanya na kaupata Maisha Maisha ya furaha kwa kiwango cha kuridhisha. Chaguzi sahihi kama zikifanywa kwa dhamira ya dhati, zinaweza kuleta hamasa tele na kuzuia hali ya kuvunjika moyo. Mawazo ya matarajio mema ni chaguzi bora kwa ajili ya kuhifadhi afya yetu ya kiakili na kufikia malengo yetu.
Nguvu ya Tumaini, Julian Melgosa
0 Comments