Siku moja Yesu akiwa amepumzika  karibu na  Kisima . Wanafunzi wake walikua wameenda  mjini kununua chakula. Anatokea mwnamke Wa nchi ya Samaria(watu wasopatana na waisraeli or wayahudi)Yesu amwambia: ‘Nipe maji ninywe.’ Mwanamke anashangaa sana kusikia hivyo. Unajua sababu? Yesu ni Myahudi, na mwanamke ni Msamaria. Na Wayahudi wengi hawapendi Wasamaria. Hawataki hata kusema nao! Lakini Yesu anapenda watu wa namna zote. Amwambia mwanamke : ‘Wewe ukimjua anayekuomba maji, ungemwomba akupe maji yanayotoa uzima.’ ‘Bwana,’ mwanamke asema, ‘kisima ni kirefu, na huna ndoo. Utapata wapi maji hayo yanayotoa uzima?’ ‘Ukinywa maji ya kisima hiki utaona kiu tena,’ Yesu amweleza. ‘Lakini maji nitakayotoa yanaweza kumfanya mtu aishi milele.’ ‘Bwana,’ mwanamke asema, ‘nipe maji hayo! Nisione kiu tena. Nisije tena huku kuteka maji.’ Mwanamke huyo anadhani Yesu anasema maji halisi. Lakini anasema juu ya kweli ya Mungu na ufalme wake. Kweli hiyo ni kama maji yanayotoa uzima. Inaweza kumpa mtu uzima wa milele. Sasa Yesu anamwambia mwanamke hivi: ‘Nenda kamwite mume wako urudi.’ ‘Sina mume,’ anajibu. ‘Umejibu sawa,’ Yesu asema. ‘Lakini umekuwa na waume watano, na yule uliye naye sasa si mume wako.’ Yule mwanamke astaajabu, kwa sababu yote hayo ni kweli. Yesu alijuaje hayo? Ni kwa vile Yesu Ndiye aliyeahidiwa akatumwa na Mungu, naye Mungu anamjulisha hayo. Wakati huo wanafunzi wa Yesu wanarudi, nao wanashangaa kumwona akizungumza na mwanamke Msamaria. Twajifunza nini kwa hayo? Kwamba Yesu anapenda wat wa mataifa yote. Sisi pia tuwa hivyo. Tusidhani watu wengine ni wabaya kwa sababu ni wa taifa fulani. Yesu anataka watu wote waijue kweli inayoongoza kwenye uzima. Na sisi pia yatupasa tuwe na nia ya kusaidia watu wajifunze kweli